Monday, July 29, 2013
NANDO WA BIG BROTHER AMEFUTWA SABABU SOMA HAPA
Mshiriki
wa Shindano la Big Brother Africa toka Tanzania, Nando amefutwa
(disqualified) katika shindano kufuatia kwenda kinyume na sheria za
shindano! kwa kugombana na mwenzake elikim
Thursday, July 25, 2013
SWAZILAND WASHINIKIZA BANGI LIWE ZAO HALALI SOMA ZAIDI HAPA
Wanaharakati nchini Swaziland washinikiza bangi liwe zao halali, kwa kuwa linasaidia kipato kwa familia nyingi masikini. hvyo kama litaruhusiwa litasaidia sana vijana na familia masikini Je nini maoni yako kuhusu jambo hili? andika comment zako hapo chini
KAMA HUKUPATA NAFASI YA KUSIKIKILIZA TAMKO LA AMRI JESHI MKUU JUU YA WANAJESHI WALIOKUFA SUDAN SOMA HAPA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kushambuliwa
na kuuawa kwa vijana saba hodari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
waliokuwa wanalinda amani katika eneo la Darfur, Sudan.
Kwa hakika, Rais amesikitishwa
sana na kitendo hicho ambako wanajeshi wengine 14 wa Tanzania
wamejeruhiwa na waasi wa Sudan na ametuma salamu za rambirambi za moyoni
mwake kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kwa familia za wafiwa wote.
Aidha, Rais Kikwete anaungana na
Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za
wafiwa kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Rais pia
anaungana na Watanzania wote kuwaombea wale walioumia katika tukio hilo
waweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani
chini ya Umoja wa Mataifa.
Katika salamu zake za rambirambi
kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Adolf Mwamunynge na
familia za wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya
kuelezea mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya
vijana wetu hao ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana
ya utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta
amani katika eneo la dunia ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza
maisha yao kwa kushambuliwa na waassi.”
Rais Kikwete ameongeza kumwambia
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na familia za wafiwa ”Napenda kwa niaba ya
Watanzania wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana
wetu hao tokea walipokwenda Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika
tokea Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007,
wamefanya kazi nzuri sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na
kazi ambayo imeiletea nchi yetu heshima kubwa. Tutaendelea kuwaenzi kwa
kujivunia kazi yao.”
Amesisitiza Mheshimiwa Rais
Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi
za dhati ya moyo wangu kuomboleza vijana wetu hawa. Kupitia kwao, natuma
salamu za rambirambi kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na
wapigaji wote wa Jeshi letu kwa kupotelewa na wenzao. “
“Aidha, kupitia kwako, natuma
salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu
zao katika tukio hilo. Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza.
Wajue kuwa uchungu wao ni uchungu
wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi
Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu. Vile
vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za
marehemu. Amina”.
Kwa walioumia, Rais Kikwete
amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Naungana pia na Watanzania wenzangu
katika kuwapa pole nyingi walioumia katika tukio hilo tukiwaombea kwa
Mwenyezi Mungu wapone haraka na kuendelea na shughuli zao za ulinzi wa
amani chini ya Umoja wa Mataifa.”
Vijana hao waliopoteza maisha yao
na walioumia, walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao
walikuwa wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika Darfur
kutoka eneo la Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi
cha kilomita 20 kutoka Khorabeche saa tatu asubuhi jana, Jumamosi, Julai
13, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUWAOMBA RADHI WAPENDWA WA BLOG HII
NI matumaini yako mu wazima wa afya kabisa kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza TUNA OMBA RADHI kutokana na siku 30 kutowahabarisha wana blog wetu kutokana na sababu zlilizo kuwa nnje wa uwezo wetu LAKINI kuanzia leo tutaendelea kufahamishana kama ilivyo kuwa kawaida asanteni na endelea kututembelea kila siku kwenye blog yetu
Subscribe to:
Posts (Atom)