Penny afunguka ukweli wa mambo asema yeye na Diamond wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachokifanya maishani.
Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV,Penniel
Mwingila aka Penny amesema kuwa yeye na mpenzi wake Diamond wamepeana
nafasi ili kila mmoja kutafakari anachokifanya maishani.
'kama
uhusiano wowote ulivyo,kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa
sababu nyingi.Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi,wote ni vijana na
wakati mwingine tunahitaji nafasi
kugundua vitu vipya,kuona kipi hasa unachokihitaji kwenye maisha.Unajua
ukimruhusu ndege afanye vitu mbalimbali then atajua kama 'mti huu ndio
unanifaa,mti huu haunifai.Hivyo nilihisi kwamba wote 'tulihitaji nafasi'
hivyo na mimi nakuchukua nafasi.Huwa nawambia watu kuwa vyovyote
ilivyo,yeyote atakayekuwa naye,nipo pembeni yake nikimshangilia
kwasababu ni kweli ( Diamond) ni mtu mzuri ndani.Achana na watu
wanavyomuona chizi chizi,sahau msanii unayemjua,ana roho nzuri na anajua
anachokitaka.Ni ngumu kuacha iende..kama ni rahisi kuacha iende basi
hujampenda huyo mtu'Alisema Penny.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment