Wednesday, June 26, 2013
ZIARA YA OBAMA MANUFAA DAR-ES-SALAAM
Hapo kesho tanzania inatarajia kumpokea raisi BARACK OBAMA kwa ajiri ya ziara atakayoifanya tanzania kwa muda week moja akiwa na AGENDA isemayo AFRICA POWER ikiwa na lengo la kuondoa umaskini. Kutokana na kuwepo kwa ziara hiyo ndani ya jiji la dar mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa ikiwemo usafi wa hali ya juu na kurekebishwa kwa baadhi ya barabara zilizo kuwa zina mashimo mashimo AMA KWELI MGENI KARIBU MGENI APONE.
Friday, June 14, 2013
DIAMOND KUPATA DILI KAMPUNI YA COKA NA KULIPWA ZAIDI YA MIL100
Mwanamuziki wa kizazi kipya NASIBU ABDULI aka diamond platnumz amefunguka masaa machache kupitia peoples station akidhibitisha kupata mkataba huo huku akisita sita kufunguka kiasi kamili ambacho analipwa lakini amebananishwa na kufunguka kuwa ni zaidi ya m100 anazolipwa mtu mzima platnumz na kampuni hiyo.
Thursday, June 13, 2013
KAMA WADAU WA DJ LANGA.BLOGSPOT.COM TUNATOA POLE KWA WATANZANIA KWA PIGO HILI TENAA SOMA HISTORIA YA LANGA FUPI HAPA
Msanii wa
muziki wa kizazi kipya nchini, Langa Mengisen Kileo, jana jioni amefariki katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar baada ya kuugua malaria na kisha
kujitokeza homa ya uti wa mgongo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Baba mzazi wa Langa, Mzee Mengesen Kileo amesema alimpeleka mwanaye Hospitali ya
Kinondoni maarufu ‘Kwa Dokta Mvungi’ ambapo aligundulika kuwa na malaria na
baadaye aligundulika kuwa na homa ya uti wa mgongo.
Mzee
Mengisen aliongeza kuwa, baada ya Dokta Mvungi kugundua kuwa Langa ana homa ya
uti wa mgongo ambayo ni hatari, leo(Juni 13,2013) asubuhi aliamua kumkimbiza hospitali ya
Muhimbili na kumfikishia chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.
Baba huyo wa
marehemu alizidi kuueleza kuwa, ilipofika mida ya saa kumi jioni, mwanaye
aliaga dunia.
Mipango ya
mazishi inaendelea kupangwa nyumbani kwao marehemu Mtaa wa Chato, Mikochocheni
jijini Dar.
Langa Kileo
enzi za uhai wake.
|
Langa
alizaliwa Desemba 22, 1985 jijini Dar es Salaam katika familia ya wanandoa
Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.
Alisoma
Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo,
akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na
baadaye shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda.
Baadaye
alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha
Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.
Langa
alitamba kwa nyimbo zake kama Pipi ya Kijiti, Matawi ya Juu, Gangsta na Rafiki
wa Kweli aliyoiachia juzi Jumatatu.
Langa
alikuwa ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka
2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha akiwa pamoja na Sarah
Kaisi `Shaa’ na Witness Mwijage `Witness’ ambapo walitamba na nyimbo kama
Unaniacha Hoi na Kiswanglish.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
Monday, June 10, 2013
AJALI ILOTOTOKEA JANA IFISI MBALIZI , YAJERUHI ZAIDI YA ABIRIA 15.
WATU 17 wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kuharibika vibaya kufuatia ajali iliyohusisha Gari la abiria aina
ya Toyota Hiace na Scania.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa Saba Mchana katika eneo la
Ifisi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Ifisi(ICC) Mbeya Vijijini.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema gari la abiria Toyota
Hiace lenye namba za usajili T 635 ALS likiendeshwa na Nikutusya Mwanja
likitokea Mbalizi kuelekea Songwe iliingia kwenye Trela la Scania lililokuwa
likitokea Tunduma kuelekea Dar Es Salaam.
Wamesema chanzo cha ajali hiyo
ni mwendokasi wa gari ndogo ambapo Dereva alikuwa akijaribu kulipita gari lingine
lakini mbele akakutana na Lori ambalo alipojaribu kulikwepa akaingia kwenye
Trela lake na kupinduka vibaya.
Trela hilo lenye namba za
usajili T 675 ACT likiwa linavutwa na Kichwa chenye namba za usajili T 378 AGD
halikuweza kuumia sana kutokana na kwenda kwa mwendo mdogo ambapo majeruhi wote
wamekimbizwa katika Hospitale teule ya Ifisi kwa matibabu zaidi.
Muuguzi Msaidizi wa Hospitali
Teule ya Ifisi Elimath Sanga amethibitisha kupokelewa kwa majeruhi 17 na kwamba
kati ya majeruhi hao 3 hali zao siyo nzuri sana ingawa majina yao hayakuweza
kupatikana.
Ameongeza kuwa majeruhi wengi
wameumia sehemu za kichwani na miguuni na kwamba baada ya kumaliza kupatiwa
huduma ya kwanza wataangalia ni wangapi wanaweza kuruhusiwa na wengine kulazwa.
Hata hivyo habari kutoka eneo la
tukio zimesema kuwa Kondakta wa gari dogo aliyefahamika kwa jina moja la Ayubu
alitoweka mara baada ya kutokea kwa ajali ingawa haifahamiki kama ni kurukwa
kwa akili au ni kukimbia kesi.
Tuesday, June 4, 2013
SITA WAFARIKI DUNIA SITA WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA UYOLE MBEYA, TAZAMA PICHA HAPA
Watu
sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya
Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa Hiace.
Masaki amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali T178 AAV aina ya Toyota Hiace inayofanya kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea uyole.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Maiti nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Aidha amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake watano na Mwanamke mmoja . Ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la Jiji.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa Hiace.
Masaki amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali T178 AAV aina ya Toyota Hiace inayofanya kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea uyole.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Maiti nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Aidha amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake watano na Mwanamke mmoja . Ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la Jiji.
WATOTO WAWAPA TABU WAZAZI WAO MZAZI AZIMIA BAADA YA MWANAWE KUHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KULAWITI
Mahakama ya wilaya ya Mbeya imemuhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Nsalaga Uyole jijini Mbeya baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha pili jina linahifadhiwa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nsalaga.
Mwendesha mashitaka wa Serikali Mheshimiwa Lugano Mwakilasa ameiambia mahakamani hiyo kuwa Nizra Mohamed (24) mkazi wa Uyole jijini Mbeya alitenda kosa hilo Novemba 5 mwaka jana (2012) majira ya saa 12 jioni.
Amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a 155 sura ya 16 ya marekebisho kanuni ya adhabu mwaka 2002 .
Kwa upande Serikali umeleta ushahidi wake ambao ni Askari walioipeleleza kesi hiyo pamoja na Daktari na binti aliye fanyiwa kitendo hicho
Awali binti huyo ameieleza Mahakamani hiyo kuwa Novemba 5 mwaka jana majira ya saa 12 jioni alivamiwa na mshitakiwa ambaye ni fundi Mwashi Katika eneo la Nsalaga ambapo mshitakiwa huyo alimkamata kwa nguvu na kumpeleka ndani ya nyumba iliyokuwa iaendelea kujengwa (pagara) kisha kumlawiti na kumsababishia maumivu makali hali iliyopelekea kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo Daktari Satumani aliyemfanyia uchunguzi Binti huyo amethibitisha mbele ya mahakama hiyo kuwa binti huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kinyama ambapo alimpa tiba katika hospitali ya Mkoa jijini Mbeya.
Mashahidi wengine akiwemo Askari Polisi amesema kuwa awali mshitakiwa alikili kosa hilo mbele ya kiapo cha Polisi kituo cha kati Mbeya ambapo mara baada ya uchunguzi kukamilika waliifikisha kesi hiyo mahakamani.
Aidha mshitakiwa huyo alileta mashahidi wawili ambao ni mafundi waashi ambao kwa pamoja walieleza mahakama hiyo kuwa hawa kujua nini kinacho endelea mahakamani hapo.
Baada ya mahakama hiyo chini ya hakimu Gilbert Ndeuruo kuridhishwa na ushahidi kwa pande zote mbili ambapo aliamuru mshitakiwa huyo kutumikia kifungo Cha miaka 30 jela ili iwefundisho kwa wengine.
Pamoja na kupatiwa nafasi ya kujitetea mshitakiwa alishindwa kutoa utetezi wake ambapo ilionekana akijikanyaga mahakamani kwa kusema kuwa hakumbuki kama alimlawiti au kumbaka mwanafunzi huyo hali iliyo mpa fursa Hakimu Ndeuruo kutoa adhabu ya miaka 30 Jela.
Hata hivyo ndugu na jamaa wa karibu na mshitakiwa waliangua Vilio na wengine kuzirai akiwepo baba mzazi wa mshitakiwa pia mke wa mshitakiwa aliye kuwa na kichanga hali iliyo pelekea wa huduma wa mahakama kufanya kazi ya kuwa tuliza watu hao.
Subscribe to:
Posts (Atom)