Watu
 sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya 
Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mbeya.
Kaimu
 Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali
 hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa 
Hiace. 
Masaki amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina 
la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali T178 AAV aina ya 
Toyota Hiace inayofanya kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa
 ikitokea Sokomatola kuelekea uyole.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Maiti
 nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria 
katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
 jijini Mbeya.
Aidha amesema majeruhi sita wamelazwa katika 
hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake watano na Mwanamke mmoja . Ambao 
mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.
Chanzo
 cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni  mwendo kasi wa Magari hayo na wito 
ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili 
kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la 
Jiji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment