Social Icons

Pages

Monday, June 10, 2013

AJALI ILOTOTOKEA JANA IFISI MBALIZI , YAJERUHI ZAIDI YA ABIRIA 15.


WATU  17 wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuharibika vibaya kufuatia ajali iliyohusisha Gari la abiria aina ya Toyota Hiace na Scania.

Ajali hiyo imetokea  jana  majira ya Saa Saba Mchana katika eneo la Ifisi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Ifisi(ICC) Mbeya Vijijini.

Mashuhuda  wa ajali hiyo wamesema gari la abiria Toyota Hiace lenye namba za usajili T 635 ALS likiendeshwa na Nikutusya Mwanja likitokea Mbalizi kuelekea Songwe iliingia kwenye Trela la Scania lililokuwa likitokea Tunduma kuelekea Dar Es Salaam.

Wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari ndogo ambapo Dereva alikuwa akijaribu kulipita gari lingine lakini mbele akakutana na Lori ambalo alipojaribu kulikwepa akaingia kwenye Trela lake na kupinduka vibaya.

Trela hilo lenye namba za usajili T 675 ACT likiwa linavutwa na Kichwa chenye namba za usajili T 378 AGD halikuweza kuumia sana kutokana na kwenda kwa mwendo mdogo ambapo majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitale teule ya Ifisi kwa matibabu zaidi.

Muuguzi Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimath Sanga amethibitisha kupokelewa kwa majeruhi 17 na kwamba kati ya majeruhi hao 3 hali zao siyo nzuri sana ingawa majina yao hayakuweza kupatikana.

Ameongeza kuwa majeruhi wengi wameumia sehemu za kichwani na miguuni na kwamba baada ya kumaliza kupatiwa huduma ya kwanza wataangalia ni wangapi wanaweza kuruhusiwa na wengine kulazwa.

Hata hivyo habari kutoka eneo la tukio zimesema kuwa Kondakta wa gari dogo aliyefahamika kwa jina moja la Ayubu alitoweka mara baada ya kutokea kwa ajali ingawa haifahamiki kama ni kurukwa kwa akili au ni kukimbia kesi.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII

Sample Text

WASILIANA NA DJ LANGA KUPITA SALUMUJUMA9@GMAIL.COM AU 0769523120 0716906250

Sample Text

AMINI KILE UNACHOKIFANYA DAIMA USIKATISHWE TAMAA NA MTU ENDELEA KUSHOW LOVE NA HII BLOG