Social Icons

Pages

Friday, May 31, 2013

WATOTO JIJINI MBEYA WAACHA SHULE NA KUJIAJIRI KUBEBA MATOFARI KWA PICHA ZAIDI ANGALIA HAPA




WATOTO WADOGO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA CHINI YA 10  KUSHOTO MTOTO COLYNS JOHN MIAKA 8 MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI IKUTI JIJINI MBEYA NA LUSHINDIHO SIMKONDA MIAKA 10 HUYU HASOMI KABISA SHULE HAPA WAMEAJIRIWA KUBEBA TOFARI KWA UJIRA WA SHILINGI 30 TU KWA TOFARI MOJA

WANANCHI KATA YA IYUNGA MTAA WA IKUTI JIJINI MBEYA WAILALAMIKIA SERIKALI TAZAMA PICHA ZOTE HAPA





Wananchi wa Kata ya Iyunga mtaa wa IKuti  jijini mbeya wamelalamikia kitendo uongozi wa jiji la mbeya kushindwa kuzuia hali ya uchafu katika eneo la soko la Ikuti jijini

          Licha ya kuwepo kwa shughuli za kimaendeleo hasa soko na shughuli nyiingine hali imekuwa mbaya katika eneo la soko hilo kutokana na kuwepo kwa mirundikano ya uchafu katika ya soko hilo.

          Wakizungumza juu ya kuwepo kwa hali hiyo  wananchi wa maeneo hayo wamedai kuwa takataka zilizo jazana katika eneo hilo la soko linahatarisha afya za wakazi wa eneo hilo kutokana kuwepo na huduma muhimu kama soko ambako kunauzwa vyakula na mahitaji mengine.

        Mmoja wa wakazi hao ndugu  Janneth Mbukwa amesema kuwa kwa muda mrefu sasa takataka hizo zimekuwepo eneo hilo licha ya wafanyabiashara wa eneo hilo pamoja na baadhi ya wananchi kutoa taarifa sehemu husika ili kulifanyia kazi suala hilo.

        Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa uchafu huo  kwa muda mrefu bado mawakala wa kutoza ushuru wamekuwa wakikusanya michango kama kawaida    Licha ya kuwepo kwa hali hiyo ambayo ni adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

        Amesema tatizo kubwa lililopo katika eneo hilo ni harufu mbaya inayo toka eneo hilo ambapo kwa asilimia kubwa huathiri shughuli  zilizopo katika eneo hilo ambapo zaidi ya vibanda 20 vya mama ntilie  vipo eneo hilo la ghuba la taka hali ambayo imefanya wateja wao kuwa na hofu juu  ya

MWILI WA MANGWEA KUWASILI KESHO TANZANIA " KWA NIABA YA WANA BLOG HII R.I.P NGWEA"

Mwili wa marehemu ALBAT MANGWEA unatarajiwa kuwasili kesho bongo mida ya saa nane mchana huko dareesalaam na kusafirishwa kwenda morogoro kwao kwa mama yake mzazi. kwa niaba ya wapenzi wa blog yaDJ LANGA.BLOGSPOT.COM tunapenda kuwapa pole watanzania wote na ndugu na jamaa kwa msiba huu mkubwa uliotufika hapo juzi uliotokea huko afrika ya kusini huku madkatari wa huko hawajatoa ripoti ya chanzo ya kifo chake tutakujulisha endapo majibu yatakuwa yashatoka.

Tuesday, May 21, 2013

ULE USEMI USEMAO' KIFO CHA PANZI FURAHA YA KUNGURU" IMEDHIHIRIKA MARA BAADA YA KUTOEA KWA AJARI YA GARI LA MAFUTA LA LAKE OIL HUKO JIJINI MBEYA TAZAMA PICHA ZOTE HAPA

Ajari hiyo imetokea maeneo ya mlima nyoka hapo juzi huku wakazi wa maeneo hayo wakinufaika vilivyo kwa kujizolea mafuta kama maji.

MAKAMANDA WA POLISI MIKOA YA KIKANDA, WAKUTANA JIJINI MBEYA, KUJADILI HALI YA UHALIFU KWA BAADHI YA POLISI.

MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu  ikiwa na kuweka mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.

Mkutano  huo unafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya usalama na uhalifu wa maeneo katika  Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya  .

Akizungumzia mikakati hiyo, Mwenyekiti wa Mkutano  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo.

Amesema Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu moja hivyo mkutano huu utasaidia kwa wajumbe kubadilishana  na kupeana uzoefu wa kazi,’alisema

Aidha, amefafanua kuwa  jeshi la polisi hivi sasa kupitia baadhi ya askari   limekuwa likikumbwa na matukio ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali za uhalifu.

Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani.

Amesema mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia njia nyingi kufanya uhalifu na kukimbilia mikoa ya jirani  hivyo  mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda pamoja na wakuu wa upelezi utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao uliopo



Mkutano huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza kufanyika Mkoani Iringa na  wapili ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio mapya.


Monday, May 20, 2013

KALA JEREMIAH "SITAKI SAPRISE KWENYE HAPHY BIRTHDAY YANGU"

Rapa kala jeremiah  aka mr dear god amefunguka kuwa kesho tarehe 21  ni siku yake ya kuzaliwa. Huku akiwaomba watu wake wote wa karibu wasimfanyie saprise yoyote katika siku hiyo. Akitaja sababu kubwa ya kutosherekia tena siku yake ya kuzaliwa ni kutokana na siku hiyo yake ya kuzaliwa ilikuwa siku ambayo yalitokea maafa makubwa sana tanzania ambapo meli ya mv bukoba ilizama  na kuuwa maelfu ya watanzani      kwaanzia siku hiyo kala amekuwa akiitumia siku hiyo kama siku ya kuwakumbuka waafa wote waliopoteza maisha katika siku hiyo.

Wednesday, May 15, 2013

TETESI ZA MATONYA KUKUTAZWA KUFANYA SHOO YA LADY JAY D

 Tetesi zinaweza kuwa za ukweli au pengine zikawa ni story za kujitungia
Lakini tetesi zinasema kuwa Matonya alipigiwa simu na wazee wa fitna mara tu waliposkia kluwa atashiriki onyesho la miaka 13 ya JayDee, wakamwambia aachane na hiyo show na kuwa watampa hela ambayo angelipwa kwenye show hiyo.

Na pia wangemuandalia show yake mwenyewe kubwa zaidi ya hiyo miaka 13 ya JayDee
Hizo ni fununu, ambazo hazina uhakika.
Lakini tukirudi upande wa Matonya ambae alishapokea mpaka malipo ya awali na kukubali kufanya show baadae akachomoa ni kama ifuatavyo.

MATONYA: Kaka kumbe tarehe ni lini kumbe:

CAPTAIN:    Ni Ijumaa tar 31 May 2013 kaka mwezi ujao. Tutakuwa na Linah, Jay, Barnaba, Matonya, TID, hamza Kalala

MATONYA: Kaka kumradh sana kuimba na band kwasasa sitoweza manake mtaitaji mandalizi makubwa ili nifanye kazi vzr_ningeomba nitizamwe ktk kazi ingine bro kumradh sana

CAPTAIN: Du! Nshatangaza ilikuwa kaka lakini sawa. Je ntapata ile hela kka nilipe wengine ndg yangu

MATONYA: Aisee hata nimekosa raha kukujuza iliswala br_kesho satano mtampa yule rafkiangu anaitwa pizon_walikuja kuleta ile pesa yagari kwaio wataileta apo apo oficen

CAPTAIN: Sawa kaka usijali, Nitashukuru akiileta ili huku nisipate lawama
MATONYA: ok bro

Mara kimyaaaaaaa....... baada ya siku mbili tatu maongezi yakaendelea

CAPTAIN: Naam kaka mzigo haujaletwa. Tafadhali ileteni tu hiyo hela ya watu kaka mi napewa lawama isitoshe we ni ndugu yangu usikubali hela ndogo iharibu.

MATONYA: Gadna aiwezi kuwa ivyo_kuna mapungufu kidgo nayaweka sawa uipate kumradh sana brother

CAPTAIN: Asante

Siku ikapita tena

MATONYA: Kaka kdg kunamisteki nimecheza,, lakini wiki hii haitapita mtakuona bro nimekwama kaka lakini ntajua cha haraka

CAPTAIN: Sijaelewa kaka ni laki **** tu kunirudishia nduguyo nilipe wasanii wengine kwani kuna tatizo au

MATONYA: Bro naskia haya - skutaka hata kuku2mia msg mlitaka ni2we namzigo 2 ila kunambio kdg zimekwamisha nikaona bora kukujuza kuliko kukaa kimya bro tatizo haliwezi

CAPTAIN: Sawa we ni ndugu yangu, basi nisaidie tu irudi hiyo advance niliyokupa ili uniepushe na lawama huku kaka. Au niende kwa bimkubwa Tanga nikalalamike? Ha haaaa haaa

CAPTAIN: Fanya hivyo mdogo wangu nilitaka uwepo ktk show kwa upendo tu lakini haijawa, basi nisaidie tu kurudisha hiyo advance maana nadaiwa na wasanii wengine niwape. Au sio?

MATONYA: Kaka nibendi ndio haya yangu kwasasa nastaki kuharibu kaziyako bora niwe mkweli.. Naswala lako halitoki kichwani bro

CAPTAIN: Sawa jamaa yangu, basi nisaidie ile advance irudi ili niweke mambo sawa huku, mimi sina mdhamini mpaka leo aliyetoa hela, najitegemea tu mfukoni, naomba nirudishie nilipe wengine..Au namoro matonya we ni ndugu yangu?

MATONYA: Sawa brother mtalisimamia soon nikuweke sawa sawa brother - akuna litakalo shindikana kaka amini 2

CAPTAIN: Utarudisha lini nipe uhakika kaka, niko na shida

Adavance ilitoka tangu mwishoni mwa mwezi April
Mazungumzo ndio kama hayo mmeyasoma
Mpaka blog inaingia mitamboni leo, advance haijarudishwa na hakuna jibu la kueleweka.

Wazee wa fitana kama zile tetesi ni kweli kuwa mmemzuia Matonya asifanya hii show ya miaka 13 ya JayDee, na hela ameshaitumia! Kwanini msimsaidie kuirejesha mambo yaishe??

Source:www.ladyjaydee.blogspot.com/

BONGO STAR SEARCH IMERUDI TENA 2013

Mara baada ya mashindano maalfu bongo katika kuibua vipaji mbali mbali "bongo star search" kushika kasi mwaka jana imerudi tena mwaka huu. Jaji mkuu madam LITA amufunguka kuwa michakato iko mbioni kuanza kupita kila mkoa kuwatafuta washiriki.

Thursday, May 2, 2013

KILIMANYARO MUSIC AWARD LEO TUNAANZA NA LINEX KUMPIGIA KURA MAELEZO HAPA

Linex libenga amechaguliwa kugombania tuzo ya mtunzi bora wa mashairi bora na msanii wa pop na nk lakini kama unataka kumpigia kura nendasehemu yako ya ujumbe mfupi andka kill kwa herufi kubwa acha nafasi  AF4 kwenda namba 15345 kuwa mtunzi bora wa mashairi.

PROFESA JAY KUMUUNGA MKONO NIKI WA PILI

Masanii nguli wa bongo fleva prof jizoo amefuguka kwa kuandika baadhi ya mstari wa niki mbishi usemayo "DEMU NINIYE MTAKA NI DEMU WA KICHAGA JIONI ANIULIZE UMEINGIZAGA SH NGAPI katika akaunt yake ya twita.  Baada ya niki mbishi kuiona hiyo twit amefunguka na kusema amefurahi kuona mwanamziki mkubwa kama profesa j kukubali baadhi ya mistari yake.

WANAWAKE BONGO MOVIE VIMINI TENA BASI

Wanawake waigizaji bongo hawaruhusiwi tena kuigiza filamu wakiwa wamevaa vimini kwenye movie yoyote tena. Kupitia bodi ya filamu tanzania imeona ilivalie nyuga suala hili la wanawake waigizaji kuvaa vimini kwani wanavunja maadili ya jamii. Saimoni mwakifwamba amekiri kabisa na ameliunga mkono suala hilo huku akisema sheria mpya hataruhusu kabisa kumuona mwigizaji wa kike kuvaa vimini endapo kama yoyote atavunja sheria hiyo basi hatua kali itachukuliwa dhidi yake na alimalizia kwa kusema saula hilo litasimamiwa na waziriri wa habari na michezo dr fenera mkangara.
 

Sample text

ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII

Sample Text

WASILIANA NA DJ LANGA KUPITA SALUMUJUMA9@GMAIL.COM AU 0769523120 0716906250

Sample Text

AMINI KILE UNACHOKIFANYA DAIMA USIKATISHWE TAMAA NA MTU ENDELEA KUSHOW LOVE NA HII BLOG