MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda,
wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu ikiwa na kuweka
mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na
taratibu za kazi.
Mkutano huo unafanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya
usalama na uhalifu wa maeneo katika Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma,
Njombe na Mbeya .
Akizungumzia mikakati hiyo, Mwenyekiti wa
Mkutano Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile
alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa
unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa
watendaji wa jeshi hilo.
Amesema Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama
hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu moja hivyo mkutano huu utasaidia
kwa wajumbe kubadilishana na kupeana uzoefu wa kazi,’alisema
Aidha, amefafanua kuwa jeshi la polisi
hivi sasa kupitia baadhi ya askari limekuwa likikumbwa na matukio
ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali za uhalifu.
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa
mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao
hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu
pamoja na ajali barabarani.
Amesema mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia
njia nyingi kufanya uhalifu na kukimbilia mikoa ya jirani hivyo
mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda pamoja na wakuu wa upelezi
utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao uliopo
Mkutano huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza
kufanyika Mkoani Iringa na wapili ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba
wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio mapya.
No comments:
Post a Comment