Mlinda mlango bora Tanzania Juma Kaseja amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga kwa dau la Sh Milioni 40.Kaseja ametia wino kwenye mkataba huo akiwa na vigogo wa 
Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na Seif Ahmed ‘Magari’ mbele 
ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala jijini Dar es Salaam.
 Kaseja atakuwa klabu moja na makipa wawili aliowahi kufanya nao 
kazi Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
Hii
 inakuwa mara ya pili Kaseja 
kusajiliwa Yanga, baada ya awali kusajiliwa miaka mitatu iliyopita 
akitokea Simba SC
 ambako baada ya msimu mmoja wa Mkataba wake kuisha alirejea Msimbazi. 
Alitemwa na simba wakati huo kwa sababu ya kiwango kushuka.
 Yanga SC 
itanufaika na uzoefu wake katika game za kimataifa na 
inataka inufaike naye katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment